Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera Hamimu Mahamudu
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Kagera wameombwa kuendelea kuhimiza amani kwa waumini wao ili kuwa na ustaarabu wa kumjua Mungu ikiwemo kuishi na watu vizuri na kuwaombea viongozi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 2, 2019 na Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera Hamimu Mahamudu katika hafla ya kuMpongeza Mzee Twail Ismail Tabilane aliyerejea kutoka Makka Saudi Arabia kuhiji iliyofanyika wilayani Misenyi Mkoani Kagera .
Mahamudu amesema nchi ya Tanzania licha ya kuendelea kuwapokea wageni kutoka sehemu tofauti lakini bado ni kisiwa cha amani hivyo amani ili iendelee kuwepo, lazima viongozi wa dini waelekeze kwa waumini wao ili kusisitiza amani hiyo izidi kutawala.
Amesema amani ni tunu kubwa hivyo ni vyema itunzwe na kuenziwa huku akiwaomba viongozi wa dini ,waumini wamuombee sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya na kutaja kufurahishwa na uamzi wake wa kuwaita watendaji wa kata nchi nzima Ikulu kwa ajili ya mazungumzo ya kuwaletea maendeleo wananchi.
Mahamudu amewataka viongozi wa dini na waumini wao kuwa na ustaarabu wa kumjua Mungu ikiwemo ustaarabu wa kuishi na watu vizuri lakini na kuifanya dunia iwe mahali bora pa kuishi.
"Nimeguswa sana na umoja huu wa waumini wa dini ya kiislamu na wasiokuwa waumini wa dini hii katika matukio mbalimbali hasa ya kidin, hakuna ubaguzi wala hamchagui, umoja huu na ushirikiano huu naomba uendelee amesema’’,amesema.
Katika hatua nyingine Katibu huyo amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Social Plugin