Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASKOFU MKUU JIMBO LA DAR ES SALAAM RUWA’ICHI ATOLEWA ICU.....APELEKWA WODI YA KAWAIDA


Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Ruwa’ichi, hali yake imeendelea kuimarika na sasa amehamishiwa katika wodi ya kawaida kutoka katika chumba cha ICU.


Hayo yameelezwa leo Jumatatu Septemba 16, 2019 katika taarifa ya kitengo cha uhusiano cha taasisi ya Mifupa(Moi) iliyosainiwa na Patrick Mvungi.

“Jopo la wataalam saba wanaomhudumia Ruwai’chi limeamua kumhamisha baada ya kujiridhisha na maendeleo ya afya yake.”

“Limefanya uamuzi huo leo asubuhi baada ya kufanya tathmini ya vipimo pamoja na taarifa mbalimbali za maendeleo yake tangu alipopokelewa Moi na kufanyiwa upasuaji Septemba 9, 2019,” inaeleza taarifa hiyo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com