Diwani wa Mwanga Kaskazini(ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Revocatus Chipando maarufu “Baba Levo“ ameongezewa kifungo Gerezani na sasa atatumikia kifungo cha Mwaka 1 na siku 2 badala ya Miezi 5 ya awali.
Hukumu hiyo imetolewa jana Septemba 10, 2019 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma, baada ya kushindwa rufaa yake ya kupinga hukumu ya awali.
Baba Levo alikata rufaa katika mahakama hiyo kupinga adhabu ya awali ya miezi mitano, kwa kosa la kumshambulia trafiki, F.8350 PC Msafiri Mponela.
Katika hukumu ya awali Baba Levo alitiwa hatiani kwa kifungu namba 240 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 chapisho la mwaka 2002 na hukumu yake kutolewa Alhamisi Agosti 1, 2019, katika mahakama ya Mwanzo Mwandiga na Hakimu Mkazi Florence Ikolongo.
Social Plugin