Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWILI WA MCHEKESHAJI MAARUFU BOSS MARTHA WAZIKWA DAR


Mwili wa mchekeshaji maarufu nchini Tanzania(Stand Up Comedian) aliyepata umaarufu kupitia Kipindi cha Cheka Tu kinachoongozwa na Coy Mzungu, Boss Martha umezikwa leo Kinyerezi jijini Dar es Salaam baada ya kufanyiwa ibada nyumbani kwao Kivule.

Mchekeshaji huyo amefariki wiki hii jijini Dar es Salaam ambapo imeelezwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa uti wa mgongo uliosababisha malaria kali na kupelekea kifo chake.

Martha ambaye ni mchekeshaji aliyekuwa akifanya 'Stand Up Comedy', alipata umaarufu kupitia Kipindi cha Cheka Tu kinachoongozwa na Coy Mzungu. Mchekeshaji huyo aliaga dunia usiku wa kuamkia Jumatano, Septemba 11 jijini Dar es Salaam.

Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kiume aliyezaa na msanii wa Bongo Fleva, Mbwana Yusuph Kilungi almaarufu Mbosso ambapo kabla ya kifo chake, walidumu kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka mitano.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com