Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM MISENYI YAVUNA WANACHAMA WAPYA...WAMO VIONGOZI WA ACT WAZALENDO NA CHADEMA

Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Kagera Ilidephonce Vedasto Murokozi na aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Bubale katika kata ya Kakunyu Joseph William Azine (CHADEMA) wamejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi hao wamejiunga CCM na kupokelewa na Katibu wa CCM wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera Hassan Moshi leo Ijumaa Septemba 13,2019 katika viwanja vya CCM kata ya Kakunyu.

Moshi amesema viongozi hao waliorejea katika chama hicho hawana budi kuendana na kasi ya Rais Magufuli katika kuhakikisha taifa na wananchi wawatumikiao wanakuwa na maendeleo endelevu.

Mbali na kumpokea Ilidephonce Vedasto Murokozi na Joseph William Azine,Moshi pia amewapokea wanachama wengine wapya na kuwapatia kadi za chama hicho huku akisisitiza akina mama kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za chama na kuacha dhana ya kuwa wanaume ndiyo wanao uwezo wa kuongoza peke yao.

Katibu huyo amesema wanachama hao wapya waliorejea na kupokelewa rasmi leo walirejesha kadi za vyama vyao Agosti 8, 2019 na kuwaomba wananchi na viongozi wa chama hicho kuwapokea kwa mikono miwili na kuwapa haki sawa na mwanachama aliyeishi miaka 30 ndani ya chama hicho.

Hata hivyo amewataka viongozi hao wapya kufuata miongozo ,sheria,na Kanuni za chama hicho ili kulinda na kukiimarisha chama.

Naye Katibu Mwenezi CCM wilaya ya Misenyi Kamuzora Coronery amewapongeza wanachama hao wapya na kuwahimiza kuwatumikia wananchi wao vyema ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli.

Nao Joseph William na Ilidephonce Vedasto Murokozi wameaahidi viongozi hao wa wilaya kuhakikisha wanafuata miongozo, sheria ,kanuni za chama hicho kwa asilimia mia moja.
Katibu wa CCM wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera Hassan Moshi akizungumza wakati wa kupokea wanachama wapya wa CCM akiwemo Aliyekuwa Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Kagera Ilidephonce Vedasto Murokozi na aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Bubale katika kata ya Kakunyu Joseph William Azine (CHADEMA).Picha zote na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Katibu wa CCM wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera Hassan Moshi akikabidhi kadi ya CCM kwa Joseph William.
Katibu wa CCM wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera Hassan Moshi akikabidhi kadi ya CCM kwa akikabidhi kadi kwa Joseph William Ilidephonce Vedasto.
Zoezi la kukabidhi kadi za CCM likiendelea.
Wanachama wapya wa CCM wakiapa.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Kagera Ilidephonce Vedasto Murokozi (kulia) na aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji cha Bubale katika kata ya Kakunyu Joseph William Azine (CHADEMA) wakionesha kadi za CCM baada ya kujiunga CCM.
Wanachama wapya wa CCM wakionesha kadi baada ya kujiunga leo
Mwenyekiti wa serikali ya kijji Kakunyu Anajoyce Byabato ni akiongea na wanachama wapya wa CCM.
Katibu mwenezi CCM wilaya ya Misenyi Kamuzora Cornery akizungumza wakati kuwapokea wanachama wapya wa CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com