Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewakuta na kesi ya kujibu viongozi 9 wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) akiwemo Mwnyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wao.
Washtakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa kufanya maandamano bila kibali, kushawishi wananchi kuichukia Serikali na uchochezi, matukio yanayodaiwa kufanyika Februari 16 mwaka 2018 wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni.
Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Social Plugin