Na Amiri kilagalila-Njombe
Halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe inaongoza kwa kuwa na asilimia 53.6% ya udumavu kimkoa kutokana na ukosefu wa lishe bora kwa jamii hususani watoto licha ya kuwepo kwa chakula cha kutosha mkoani humo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata Mwenda amebainisha hayo katika tamasha la tatu la maonyesho ya utamaduni lililofanyika katika uwanja wa sabasaba mjini Njombe,na kuwataka wadau wa utamaduni kushirikiana na serikali kutoa elimu dhidi ya lishe bora.
“Katika eneo letu tuna shida sana ya udumavu,sisi kimkoa Tanzania nzima tunaongoza kwa lishe duni,udumavu kwetu ni asilimia 53.6% haya maneno sio mazuri maskioni na ninaamini kituo chetu cha utamaduni kwa kushirikiana na wadau wengine mtaweza kufanya jambo hili la utapiamlo kuwa historia”alisema Iluminata Mwenda
Katika hatua nyingine Bi.Mwenda amesema mkoa wa Njombe bado unaongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuwa na asilimia 11% kitaifa na kuiagiza jamii kuhakikisha haisababishi maambukizi mapya.
“Sisi kitaifa Njombe ukimwi ni 11% ni agize kwamba kila mmoja katika nafasi yake tuhakikishe hatupati maambukizi mapya,na wale ambao wameshaambukizwa kwa bahati mbaya waendelee na tiba,na katika maonyesho haya inatakiwa tuhakikishe tunatoa elimu kwa kutumia ngoma, nyimb,maigizo hata kwa kwenda radioni kuhakikisha tunapiga vita ukimwi ili tuwe salama”aliongeza Bi.Mwenda
Stiven Mligo ni mkurugenzi wa kituo cha sanaa na utamaduni Njombe Tasunjo,anasema wameanzisha matamasha hayo mkoani Njombe ili kudumisha utamaduni wa mtanzania na wananjombe pamoja na kuendelea kuiunga mkono serikali katika mambo mbali mbali ya kijamii.
“Sisis tumeanzisha matamasha haya kwasababu kubwa mbili,lakini moja ni kudumisha na kuenzi utamaduni wa wananjombe na Tanzania kwa ujumla,lakini jambo la pili licha ya kuisadia serikali lakini tunachotaka ni kudumisha sanaa hizi zinazofanywa na wanautamaduni kwa kuwa wana kazi za mikono yao”alisema Stiven Mligo
Godeln Nyagawa na Rehema nyenzi ni miongoni mwa wanavikundi wa ngoma za utamaduni waliohudhuria katika tamasha hilo,wanasema kupitia sanaa zao wanayo nafasi kubwa ya kuibadilisha jami.
Social Plugin