Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA JACQUES CHIRAC

Jacques Chirac, rais wa zamani wa Ufaransa ambaye miaka yake ya baadaye ilikabiliwa na kashfa za ufisadi amefariki akiwa na umri wa miaka 86.

Chirac alifariki mapema leo asubuhi akiwa na familia yake , mwanawe wa kambo aliambia chombo cha habari cha AFP.

Bwana Chirac alihudumu miaka miwili kama rais wa Ufaransa na kuliongoza taifa lake kuingia katika sarafu moja ya Ulaya.

Bunge la Ufaransa limempatia heshima ya dakika moja kwa kunyamaza.
Rais wa tume ya Ulaya na waziri mkuu wa zamani wa Luxembourg Jean-Claude Juncker amesema kwamba aiskitishwa na habari hiyo.

Ulaya haikupoteza tu kiongozi muhimu ,bali idara ya urais itamkosa rafiki mkubwa, msemaji wake alinukuliwa na bwana Juncker akisema.

Kashfa ya Ufisadi

Mabadiliko makubwa ya kisiasa yaliofanywa na bwana Chirac ilikuwa kupunguza muhula wa rais kutoka miaka saba hadi mitano.

Alionekana kama mpinzani mkuu wa uvamizi wa Marekani nchini Iraq 2003.

Alihudumu kama kiongozi wa taifa kutoka 1995 hadi 2007 huku afya yake ikidorora tangu wakati huo.

Pia alihudumu kama waziri mkuu wa Ufaransa, lakini akakabiliwa na msururu wa kesi za ufisadi .

Mwaka 2011 alihukumiwa kwa kuchukua fedha za umma alipokuwa akihudumu kama Meya.

Aliugua kiharusi 2005 na mwaka 2014, mkewe Bernadette alisema kwamba hatazungumza hadharani akidai kwamba alikuwa na matatizo ya kiakili kulingana na chombo cha habari cha Ufaransa.

Alikuwa rais wa Ufaransa aliyehudumu kwa muda mrefu baada ya kumrithi Francois Mitterrand.

Apiga vita mpango wa kutokuwpo kwa muungano wa Ulaya na kupigania katiba ya Ulaya ambayo ilikataliwa na wapiga kura ya Ufaransa.

Alizaliwa 1932, mwana wa meneja wa benki ambaye baadaye alikuwa meneja mkurugenzi wa kampuni ya Dassault.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com