Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KASHASHA APATA USHINDI MNONO NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI HALMASHAURI YA BUKOBA

Mhe. Deogratias Kashasha 

Na Lyidia Lugakila - Malunde 1 blog
Diwani wa kata Kishanje, Mhe. Deogratias Kashasha amefanikiwa kutetea tena kiti cha  Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba.


Uchaguzi huo umefanyika leo Septemba 5,2019 katika kikao cha baraza la madiwani kwa ajili ya kufunga mwaka 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Awali mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba,Mhe. Hashim Murshid Ngeze aliyataja majina ya wajumbe walioomba nafasi ya kugombea nafasi hiyo kuwa ni Bwana Deogratias Kashasha ambaye ni Diwani wa kata ya Kishanje (CCM) na Rwekaza Deusdedith diwani wa kata ya Katoma (Chadema).

Kufuatia uchaguzi huo,Mhe. Deogratias Kashasha ameibuka mshindi nafasi ya makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba kwa kupata kura 28 dhidi ya mpinzani wake Rwekaza Deusdedith aliyepata kura kura 7 ambapo jumla ya wapiga kura walikuwa ni 35.


Kashasha amewashukuru madiwani hao kwa kumchagua kutetea kiti hicho na kuahidi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu ili kutekekeza ilani ya Chama Cha mapinduzi CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Kushoto ni Mhe. Deogratias Kashasha (CCM) akiwa na mgombea mwenzake nafasi ya makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Bukoba,Mhe. Rwekaza Deusdedith (CHADEMA)

Mhe. Deogratias Kashasha (CCM) akijipigia kura wakati wa uchaguzi nafasi ya makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Bukoba leo

Mhe. Rwekaza Deusdedith (CHADEMA) akijipigia kura akijipigia kura wakati wa uchaguzi nafasi ya makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Bukoba leo

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba, Mhe. Hashimu Murshid Ngeze akitoa hotuba ya katika kikao cha baraza la madiwani






Diwani kata Kyaitoke, Mhe. Asuma Bantanuka akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba  Solomon Kimilike  akihimiza masuala mbalimbali ya maendeleo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com