Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAMA AUA MTOTO WAKE KWA KUMKATA KISU SHINGONI

Mkazi wa Kijiji cha Katangara Wilayani Rombo, Philipina Donath(37) amedaiwa kumuua mtoto wake wa miaka mitano kwa kumkata na kisu shingoni kisha kujisalimisha mwenye kituo cha polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah amesema leo Septemba 2019 kuwa tukio hilo lilitokea jana katika Kijiji cha Katangara Mashati.

"Cha kushangaza mwanamke huyo baada ya kufanya mauaji ya mwanaye alijisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi Masharti na polisi walipofika nyumbani kwake walikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa chini huku pembeni mwa mwili huo kukiwa na kisu chenye damu, "amesema Kamanda Issah.

Pia, amesema polisi wanamshikilia mwanamke huyo kwa kujihusisha na mauaji hayo.

Amesema mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Na Janeth Joseph - Mwananchi
Chanzo-  Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com