Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema kila baada ya sekunde 40 mtu mmoja hujitoa uhai ulimwenguni, sababu kuu ikiwa ni kushindwa kuhimili msongo wa mawazo kutokana changamoto mbalimbali za kiuchumi, kimapenzi, na kisiasa.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ametoa takwimu hizo kupitia mtandao wao kuwa asilimia 79 ya vifo hivyo, vinatokea kwenye nchi zenye uchumi wa kati na zinazoendelea kukua.
Aidha amesema taifa la Sri Lanka limekuwa na changamoto kubwa ya watu kujiua kutokana na kushindwa kuhimili changamoto za kiuchumi na mahusiano.
Kila Septemba 10, ya kila mwaka Shirika la Afya Duniani limekuwa likiadhimisha siku ya kuzuia kujiua, hii ni kutokana na kuongezeka kwa matukio ya aina hiyo ulimwenguni kote.
Social Plugin