Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametua katika kanisa Pentecostal Power Ministry na kuamuru kukamatwa kwa Mchungaji wa kanisa Hilo Nabii Eliya Mahela kwa kosa la kuendesha kanisa bila kusajili
wa na kupiga kelele kwa Wananchi wanaomzunguka.
Uamuzi wa kukamatwa kwa Nabii Mahela umetolewa leo Jumatatu Septemba 9, 2019 na Waziri Lugola baada ya kufanya ziara katika kanisa hilo kufuatia malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa majirani dhidi ya kanisa hilo.
Amesema majirani wa eneo hilo kwa nyakati tofauti wamekuwa wakilalamika kelele zinazotoka kanisa hilo na licha ya viongozi wa Serikali kumpa onyo la kujirekebisha mchungaji huyo hakufanya hivyo.
"Ulikuwa ukiwaambia wananchi kuwa ujali na waende kokote leo kokote zimefika 40. Kokote nipo hapa na kokote hutopona," amesema Lugola.
Social Plugin