Mbunge wa Nungwi visiwani Zanzibar, Yusuph Hamis, amehoji juu ya mkakati wa Serikali katika kukabiliana na matatizo ya watoto kuokota mabomu, ili kuepusha vifo ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara jimboni kwake.
Mbunge Yusuph Hamis, amehoji swali katika vikao vya Bunge vinavyoendelea jijini Dodoma, ambapo ameomba kauli ya Serikali ili kumaliza tatizo hilo.
"Kule jimboni kwangu watoto wanaokota mabomu wakidhani chuma chakavu, mwisho yanalipuka, Serikali mnasemaje?" amehoji Mbunge wa Nungwi Yussuph Hamis.
Akijibu swali hilo Bungeni, Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi, amesema Jeshi la Wananchi Tanzania limeshatoa elimu juu ya kutookota vyuma vinavyong'aa, tangu ilipomalizika kwa vita ya Kagera.
"Baada ya vita ya Kagera, JWTZ ilitoa elimu ya kutookota vitu vinavyong'aa kwenye maeneo yaliyotiliwa mashaka, inashauriwa wananchi katika Mkoa huo wachukue tahadhari wanapoona vitu vyenye asili ya chuma." amesema Waziri Hussein Mwinyi.
Social Plugin