Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MSALABA MWEKUNDU KUSAIDIA WILAYA YA KYELA KUKABILIANA NA MAFURIKO

Wanachama wa chama msalaba mwekundu Jijini Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kitaifa mara baada ya kumaliza mkutano wao

Na Esther Macha - Malunde 1 blog Mbeya 

CHAMA cha Msalaba mwekundu Tanzania TRCS kwa kushirikiana na Serikali kimekuja na mradi wa miaka miwili unaolenga kudhibiti na kukabiliana na majanga ya mara kwa mara ya mafuriko na magonjwa ya mlipuko kuwakomboa  wakazi wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kila mwaka.

Kyela ni wilaya iliyopo mkoani  Mbeya ambayo imekuwa na changamoto ya kukubwa na mafuriko kila mwaka ambayo pia huambatana na magonjwa ya mlipuko kama vile Kipindupindu.

Akizungumza na majira mkazi wa Kyela,  Ipute Kandu alisema wanashukuru chama cha msalaba mwekundu kwa hicho kilichofanyika kwani inaweza kuwa tiba kwa wana kyela. 

Chama cha msaba mwekundu Tanzania TRSC kupitia ufadhili wa nchi ya Ubelgiji, wamekuja na mradi maalumu utakao saidia wakazi wa wilaya ya Kyela kukabiliana na Majanga hayo.

Mkurugenzi wa idara ya maafa TRCS,Renatus Mkaluka alisema kuwa katika mradi huo 
 ambao ni wa miaka miwili unalenga hasa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujiandaa kukabiliana na Mafuriko pamoja na magonjwa ya mlipuko.

Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mwalimu Claudia Kitta alieleza umuhimu wa mradi huo kwa wakazi wa wilaya hiyo na kuwataka kuutumia vizuri. 

Aprili mwaka huu 2019 wilaya ya Kyela ilikubwa na mafuriko ambayo yalisababisha vifo vya watu watano na kuacha madhara makubwa kwa wahanga wa mafuriko hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com