Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAPENZI WAUAWA KWA KUCHOMWA MOTO KWA WIVU WA MAPENZI

Mwanaume mmoja Raia wa Marekani Ashley Martin (32), amemuua mpenzi wake wa zamani pamoja na mwanaume aliyekuwa kwenye mahusino mapya na mwanamke huyo, kwa kuichoma moto nyumba waliyokuwa wakiishi wawili hao iliyopo katika mji wa Linconshore.

Inadaiwa kwamba mwanaume huyo alipanga mauaji hayo kama kulipiza kisasi kwa aliyekuwa mpenzi wake huyo wa zamani Jay Edmunds (27), pamoja na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Billy Hicks 24.

Kwa mujibu wa Afisa Upelelezi nchini humo, ameeleza kwamba Ashley alimshambulia Billy kwa kumchoma kisu katika kifua chake, wakati akijaribu kupambana nae na baada ya kutekeleza hayo alichukua petroli na kuichoma moto nyumba na kupelekea vifo vya watu watatu akiwemo yeye mwenyewe.

Aidha wakati polisi wakifanya upekuzi katika nyumba hiyo walikuta kipande cha karatasi kilichokuwa na ujumbe kutoka kwa Ashley kwenda kwa Jay, uliokuwa na maneno ya kumkashifu na kumdhihaki.

Katika tukio hilo Polisi wengine watano kutoka katika kituo cha polisi cha Linconshire, waliofika katika eneo hilo kwa ajili ya kufanya uokoaji, walijeruhiwa vibaya na moto uliolipuka wakati wakikaribia katika mlango wa mbele wa nyumba hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com