Mchezaji wa mpira wa mawe
Kundi la vijana wa Mexico linafufua mchezo wa jadi wa mpira wa mawe kwao maarufu kama 'Ulama', uliowahi kuchezwa na jamii za Aztecs, Maya na Incas.
Mchezo huo ulichezwa huko Mesoamerica zaidi ya karne tano zilizopita, kabla ya watawala wa Uhispania kuwasili katika eneo hilo mnamo mwaka 1519.
Katika mchezo huo wachezaji huvaa mikanda maalumu na vitamba vya kujifunika sehemu zao za siri na wanasukuma mpira kwa viuno vyao. Mpira unatajwa kuweza kuwa na uzito wa hadi kilo 4 na inaaminika kuwa kuna aina tofauti za mchezo huo na mara nyingi ilidhaniwa ulihusisha timu hasimu zikikabiliana ana kwa ana.
Kila upande ukiwa unasalia katika sehemu ya nusu ya uwanja na kupasisha mpira kutoka timu moja hadi nyingine pasipo kuangusha mpira, katika aina nyingine za mchezo huo ulichezwa katika eneo lililozungukwa kwa kuta za mawe lenye mduara uliomfano wa vikapu ama mpira wa vikapu.
Wakati mchezo wa Ualama unafufuliwa katika baadhi ya maeneo ya kale nchini Mexico, mji mkuu haukuwa na sehemu ya kuchezea mchezo huo hadi hivi karibuni ambapo kumejengwa eneo la kitamaduni katika sehemu ya kutupa taka katika mtaa wa Azcapotzalco. Emmanuel Kakaloti ni mkufunzi katika uwanja huo mpya “Mchezo huu ulikuwa umesahaulika, ulipinduliwa miaka 500 iliyopita lakini sasa tunaufufua”.
Na Beatriz Campos (25) ni mojawapo ya wachezaji ambaye alifafanua namna ambavyo wanawake wanashiriki katika mchezo huo, “sisi ni mashujaa wanawake kwasababu sio rahisi kila mtu kucheza na inataka mazoezi mengi,,.
Mchezo wa Ulama unaaminika kuwa tambiko za kitamaduni na wachezaji huvaa mavazi maalum na hufanya tambiko kabla ya kuingia uwanjani kwa ajili ya mchezo.