Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE AGOMA KUTOKA NDANI YA STUDIO POLISI WAKIMSUBIRI NJE



 Mbunge wa Kiharu nchini Kenya, Ndindi Nyoro amegoma kutoka ndani ya studio za Royal Media Services usiku Jumapili Septemba 8, 2019 wakati polisi wakidaiwa kumsubiri nje ya studio hizo ili wamkamate.

Mbunge huyo alidai hawezi kutoka ndani ya studio hizo kwenda nje kwa sababu kwanza hana uhakika kama waliopo nje wakimsubiri kumkamata ni polisi ama laa.

“Siwezi kujipeleka nje ya kampuni ya Royal Media Services kwa sababu sijui kama wanaoningojea ni polisi. Mimi nalala hapa kwa kiti kwenye Royal Media Services”, amesema Ndindi Nyoro.

Kuhusu kufuatwa na polisi katika studio hizo, mbunge huyo amesema, "Matukio ya leo yamenishangaza. Iwapo nina makosa, ningependa kujua ili nijisalimishe kwa polisi mimi mwenyewe."

Licha ya sababu za watu wanaodaiwa kuwa polisi kumsubiri nje ya studio hizo kwa lengo la kumkamata, Mbunge huyo amesema yeye kama mbunge wa Kiharu nchini humo ana haki ya kuzuru eneo lolote na watu wasifikirie watamtisha kwa sababu wazazi wake hawajulikani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com