Mchungaji Amos Joseph kutoka kanisa la Victoria Itobo wilaya ya Nzega mkoani Tabora amenusurika kufa baada ya kushambuliwa na kundi la vijana wasiojulikana leo alfajiri Jumamosi Septemba 7,2019 katika Manispaa ya Tabora.
Kwa Mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde 1 blog kuwa Mchungaji huyo amekutwa akiwa hoi amelala hawezi kusimama pembezoni mwa shule ya msingi Mabatini Manispaa ya Tabora mkabala na barabara kuu kutoka Kigoma kwenda Dar es salaam.
"Tumezungumza nae japo haongei sana anasema amefika Mjini Tabora akitokea Itobo wilaya ya Nzega, alikuja Tabora kumtafuta mke wake aliyetoroka nyumbani na kumwachia mtoto. Alipofika Tabora leo amekumbana na vijana wakitaka pesa,wakamshambulia kisha kuchukua pesa na simu zake",ameeleza mmoja wa mashuhuda hao.
Tayari wasamaria wema wamejitokeza kumsaidia na taratibu za kumpatia matibabu zinaendelea.
Huyu ni mchungaji Amos Joseph kutoka kanisa la Victoria Itobo,amepatikana alfajiri barabara kigoma - Dar hapa jirani na shule ya msingi Mabatini manispaa ya Tabora,ameshambuliwa kwa kupigwa sana kiasi hawezi hata kusimama,kimsingi yupo hoi.Msaada wa haraka unahitajika bado yupo hapa pembeni ya barabara amelala
Social Plugin