Straika wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa dunia katika Usiku wa Tuzo za FIFA uliohitimishwa muda mfupi uliopita Jijini Milan, nchini Italia.
Mesi amewashinda amewashinda Cristiano Ronaldo wa Juventus na Virgil van Dijk (NED) wa Liverpool alioingianao fainali.
Kwa upande wa wanawake, Megan Rapince wa Reign FC na timu ya taifa ya Marekani ndiye mchezaji bora akiwashinda Lucy Bronze (ENG) wa Olympique Lyonnais na Alex Morgan (USA) wa Orlando Pride
Tuzo nyingine zilizotolewa usiku huu ni kama ifuatavyo.
Tuzo ya Kocha Bora kwa timu za wanaume imekwenda kwa Mjerumani Jurgen Klop wa Liverpool akiwashinda Pep Guardiola (ESP) wa Manchester City na Mauricio Pochettino (ARG) wa Tottenham Hotspur.
Jill Ellis aliyekuwa akiinoa Marekani ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Timu za Wanawake akiwabwaga Phil Neville (ENG) wa England na Sarina Wiegman (NED) wa Uholanzi.
Tuzo ya Shabiki Bora imekwenda kwa Silvia Grecco wa Brazil akiwashinda Justo Sanchez wa Uruguay pamoja na Mashabiki wa timu ya taifa ya Uholanzi kwenye Kombe la Dunia kwa Wanawake.
Mbrazil Alisson anayecheza Liverpool ametwaa tuzo ya Golikipa Bora akiwapiku Ederson (BRA) wa Manchester City na Marc-André ter Stegen (GER) wa FC Barcelona.
Tuzo ya Golikipa Bora wa Kike imechukuliwa na Sari van Veenendaal wa Uholanzi aliyekuwa Arsenal sasa Atletico Madrid. Sari amewashinda Christiane Endler (CHI) wa PSG na Hedvig Lindahl (SWE) wa Chelsea / Wolfsburg.
Tuzo ya Goli Bora ( #Puskas Award ) imekwenda kwa Dániel Zsóri (HUN) kwenye mchezo kati ya Debrecen FC v Ferencváros TC [Nemzeti Bajnoskag I] Februari 16, 2019.
Zsori amewashinda Lionel Messi (ARG) - Real Betis v FC Barcelona [La Liga] - Machi 17, 2019 pamoja na Juan Fernando Quintero (COL) - River Plate v Racing Club [Argentinian Superliga] - February 10, 2019.
Tuzo ya mchezo wa kiungwana (Fair Play Award) imekwenda kwa Marcelo Bielsa pamoja na kikosi cha Liverpool .
Social Plugin