Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mfumko wa bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi Agosti ,2019 umepungua hadi asilimia 3.6% kutoka asilimia 3.7% kwa mwaka ulioishia Mwezi Julai,2019.
Mfumko wa bei wa Taifa kwa Mwaka ulioishia Mwezi Agosti ,2019 umepungua hadi asilimia 3.6% kutoka asilimia 3.7% kwa mwaka ulioishia Mwezi Julai,2019.
Hayo yamesemwa leo Septemba 9,2019 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi ,Sensa ya watu na Takwimu za Jamii Bi.Ruth Davison wakati akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya hali a mfumuko wa bei nchini.
Bi.Ruth amesema hiyo inamaanisha kuwa ,kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti ,2019 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mwezi Julai ,2019.
Hivyo,Bi.Ruth amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti ,2019 kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumuko wa bei wa bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha Mwezi Agosti,2019 zikilinganishwa na bei za Mwezi Agosti,2018.
Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizopungua bei kwa Mwezi Agosti,2019 zikilinganishwa na bei ya bidhaa za Mwezi Agosti ,2018 ni pamoja na Mafuta ya Taa kwa asilimia 2.6%,Petrol kwa asilimia 4.3%,majiko ya gesi kwa asilimia 1.4%,gharama za kufanya ukarabati wa nyumba kwa asilimia 1.7%, na bidhaa za usafi binafsi binafsi kama mafuta ya nywele kwa asilimia 1.3%.
Bi.Ruth ameendelea kufafanua juu ya mfumko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Agosti ,2019 umeongezeka hadi asilimia 3.7% kutoka asilimia 2.9 Mwezi Julai ,2019.
Hata hivyo ,Bi.Ruth amezungumzia hali ya Mfumlko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki,ambapo nchini Kenya Mfumko wa Bei kwa mwaka ulioishia Mwezi Agosti,2019 umepungua hadi asilimia 5%,kutoka asilimia 6.27 %kwamwaka uliyoishia mwezi Julai,2019.
Aidha amesema kwa upande kwa Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Agosti,2019 umepungua hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 2.6 kwa mwaka ulioishia mwezi julai ,2019
Ikumbukwe kuwa ofsi ya Taifa ya Takwimu {NBS]Ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa sheria ya takwimu ya mwaka 2015 ,pamoja na mapitio yake ya mwaka 2018 na 2019 ambapo imepewa mamlaka ya kutoa,na kusimamia sambamba na kuratibu upatikanaji wa takwimu hapa nchini.
Social Plugin