Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUCHOCHEA VUGUVUGU LA KIMAPINDUZI KATIKA USAWA WA KIJINSIA

Alphosina Ambrosi
Vijana wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa ya kusaidia jamii ikiwemo kuchochea vuguvugu la kimapinduzi katika kuleta usawa wa kijinsia.

Rai hiyo imetolewa leo Septemba 26,2019 na Mwanachama wa Jukwaa la Vijana TGNP Mtandao,Alphosina Ambrosi kwenye warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam.

Ambrosi alisema asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ni vijana hivyo ni vyema wakatumia mitandao hiyo vizuri kwa lugha nzuri kuisaidia jamii ikiwemo kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia.

"Asilimia kubwa ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ni vijana, na vijana ndiyo wanaongoza kwa 'kupost upuuzi' mitandaoni,wanatuma picha chafu na vitu vingine vingine visivyofaa katika jamii kama vile kudhalilisha wanawake",alieleza.

"Naomba vijana wabadilike,waweke vitu vya kujenga jamii ikiwemo kuweka habari,taarifa na picha za watoto na wanawake wanaofanya mambo mazuri badala kushadadia picha,habari ama taarifa zinazoleta unyanyasaji wa kijinsia",aliongeza Ambrosi.
 Mwanachama wa Jukwaa la Vijana TGNP Mtandao,Alphosina Ambrosi akizungumza leo Septemba 26,2019 kwenye warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao,Mabibo Jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanachama wa Jukwaa la Vijana TGNP Mtandao,Alphosina Ambrosi akiwasisitiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kuchochea vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Alphosina Ambrosi akisisitiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Kiongozi wa Jukwaa la Vijana TGNP Mtandao,Janeth John akizungumza kwenye warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Soma na Maendeleo,Demere Kitunga kwenye warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya SDF Foundation, Furaha Mbakile akizungumza kwenye warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Washiriki wa warsha kuhusu Matumizi ya Mitandao ya Kijamii katika vuguvugu la kimapinduzi katika usawa wa kijinsia wakati wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com