Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Bukoba Solomoni Kimilike
Na Ashura Jumapili, Bukoba.
Katika kutunza na kuhifadhi mazingira halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera kwa kipindi cha mwaka 2018/2019 kwa kishirikiana na wananchi pamoja na asasi mbalimbali imepanda jumla ya miti 1,836,342.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Solomoni Kimilike Agost 4 mwaka huu katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.
Kimilike, alisema lengo lilikuwa kupanda miti 1,500,000 ambapo miti 1,743,189 inaendelea kustawi.
Alisema wananchi wamehamasishwa kupanda miti rafiki na kutunza mazingira katika maeneo yao.
Alisema halmashauri kwa kushirikiana na tume ya Taifa ya mpango wa matumizi bora ya Ardhi wananchi wa Vijiji 8 wanaweza kupimiwa na kumilikishwa maeneo yao kwa njia ya hati miliki za kimila.
Alisema kwa kipindi cha robo hii wamepima na kumilikisha mashamba 8.
Alisema mpango wa urasimishaji shirikishi jamii wamepima viwanja 25 katika eneo la Katoro na uhamasishaji wa wananchi kuandaa mpango wa matumizi bora ya Ardhi unaendelea katika vijiji vyote.
Alisema hadi sasa Vijiji 73 vimehamasishwa kati ya Vijiji 94 vya halmashauri hiyo na zoezi linaendea kwa Vijiji vingine.
Social Plugin