KUTANA NA MNYAMA MWENYE KIYOYOZI KICHWANI


Anaitwa Tyrannosaurus rex Mnyama huyo mkubwa alihitaji njia ya kupunguza joto mwilini.

Na sasa wanasayansi wanasema kwamba mashimo mawili katika fuvu lake la kichwa yalitumiwa kama kiyoyozi ili kumwezesha dubwana huyo hatari kupunguza joto mwilini.

Mashimo hayo mawili awali yalidhaniwa kujaa misuli. Lakini kundi moja la wanasayansi linasema kuwa mashimo hayo yalikuwa na mishipa iliyomsaidia mnyama huyo kupunguza joto mwilini.

Wanyama wakubwa uhitaji mfumo maalum wa kudhibiti joto mwilini kwa kuwa joto lililopo mwilini linaweza kuadhuru katika katika joto kali.

Casey Holliday kutoka chuo kikuu cha Missouri , na wenzake walitumia vifaa vya kupima joto ambavyo hubadili joto hadi mwangaza ili kuwachugunguza mamba katika kituo cha mamba cha St Augustine mjini Florida.

Ni vigumu kupata picha ya moja ka moja kuhusu fuvu la kichwa la mamba kwa kuwa ni hatari kuwakaribia, alisema. Katika kituo hicho tulifanikiwa kupata picha na video kutoka juu.
Waligundua kwamba mamba wana mashimo ya mishipa ya damu katika mafuvu yao ya kichwa.

Joto katika mwili wa mamba hutegemea mazingira yake, alisema mwanzilishi mwenza Kent Vliet kutoika chuo kikuu cha Florida mjini gaineville.

Tuligundua kwamba wakati kulikuwa na baridi na mambo hao walikuwa wakijaribu kupata joto, vipoimo vyetu vya joto vilituonyesha maodoa makubwa ya joto katika mashimo hayo yalioipo katika paaya fuvu la kichwa m ikionyesha kupanda kwa viwango vya joto.

Na baadaye madoa hayo yalionekana kuwa meusi wakati kulikuwa na joto.

Baada ya kumchunguza dubwana huyo kwa jina Tyrannosaurus rex waligundua kwamba kwamba mnyama huyo alikuwa na na mashimo kama hayo.katika siku za nyuma wanasayansi waliamni kwamba mashimo hayo mawili yaliojaa mishima ya damu yalikuwa yakimsaidia mnyama huyo wakati anapotafuta kitu.

Hatahivyo casey anasema inashangaza kuona msuli ukitoka katika taya.
Larry Witmer, mtaalamu wa sayansi inayohusisha maumbile ya mwanadamu , wanayama na viumbe vingine vinavyoishi kama kutoka chuo cha Ohio ambaye pia alihusishwa katika utafiti huo alisema: Tunajua kwamba mbali na dubwana huyo, mamba pia wana mashimo katika paa ya fuvu lao la kichwa na mashimo hayo huwa yamejaa mishipa ya damu.

Casey anaongezea kkwamba ukiwa mnyama mkubwa kama dubwana huyu , wakati mmoja unataka kupunguza joto mwilini sawa na vile unavyohitaji joto.

Uwepo wa mishipa mingi katika fuvu la kichwa kunatoa uwezo kwa wanayama kama hawa kujipataia joto na vilevile kutoa joto hilo.

Ugunduzi huo umechapishwa katika rekodi za maumbile ya wanyama na binadamu.

Follow Paul on Twitter.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post