Basi la Kampuni ya Mwendo Haraka (Udart) maarufu 'Mwendokasi' lililokuwa likitoka Mjini kwenda Kimara Mwisho Dar es Salaam nchini Tanzania limeteketea lote kwa moto.
Tukio hilo limetokea leo usiku wa Jumapili Septemba 1, 2019 eneo la Kimara Mwisho na kusababisha adha kwa watumiaji wa usafiri huo huku watu wengi wakijitokeza kushuhudia basi hilo ambalo limetekelea lote.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Teopista Malya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema hakuna madhara kwa binadamu yaliyotokana na ajali hiyo.
Kamanda Malya amesema basi hilo lilitoka Mjini likiwa na abiria na lilipofika eneo la Kimara Mwisho walifanikiwa kushuka kabla halijateketea kwa moto.
Via Mwananchi
Social Plugin