Rais Donald Trump wa Marekani amesema mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani John Bolton amejiuzulu baada ya kumuomba afanye hivyo.
Trump alimtaka Bolton ajiuzulu Jumatatu jioni na kupokea barua ya kujiuzulu Jumanne asubuhi.
Amesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa yeye na viongozi wengine hawakukubali mapendekezo yake mengi.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Hogan Gidley aliwaambia wanahabari kuwa Trump na Bolton hawaelewani katika masuala mengi.
Social Plugin