Mpishi mmoja amekamatwa kwa kutuhumiwa kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya baada ya polisi kugundua bangi nyumbani kwake, vyombo vya habari Italia vinaripoti.
Carmelo Chiaramonte ambaye ni mpishi anayeshiriki kipindi kwenye televisheni alipatikana na mimea miwili mikubwa ya bangi na kilo mmoja ya Indian hemp, polisi inasema.
Mvinyo uliochanganywa na bangi, zaituni, kahawa, na samaki aina ya tuna pia vilikusanywa nyumbani mwake karibu na Catania huko Sicily mashariki.
Inaarifiwa mpishi huyo aliwaeleza maafisa wapolisi kwamba alikuwa anajaribu 'viungo vipya vya upishi'.
Chiaramonte amesema yeye ni mshauri wa vyakula asili kwa upishi wa kileo ", gazeti la Italia La Sicilia limeripoti.
Mpishi huyo wa miaka 50, anayeishi katika kijiji cha Trecastagni, chini ya mlima Etna ameachiwa huru huku kesi ikisubiriwa kuwasilishwa.
Chiaramonte ni mpishi katika hoteli ya Katane Palace huko Catania.
Yeye hupika vyakula vya watu wa Meditarenia kwa mujibu wa maelezo kwenye mtandao wake.
Alishiriki kipindi cha mapishi kwenye televisheni kuhusu "historia ya mazao na utamaduni wa kilimo cha Sicily", La Sicilia limeripoti.
Mojawapo ya vipindi vyake kiliitwa 'upishi uliokosa nidhamu' na 'vyakula vya kutia hamu ya tendo la ndoa', gazeti hilo limesema.
CHANZO- BBC
Social Plugin