Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA BODI YA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA AIRTEL TANZANIA, DK OMARY NUNDU AFARIKI DUNIA


Mwenyekiti  wa Bodi ya kampuni ya simu za mkononi yaAirtel Tanzania, Dk Omary Nundu, 71, amefariki dunia leo, Jumatano, Septemba 11, 2019.

Kitengo cha Mawasiliano cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam kimethibitisha kifo hicho kupitia taarifa maalum kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Waziri huyo wa zamani alifikishwa hospitalini hapo akiwa kwenye gari binafsi la wagonjwa akiwa tayari ameshafariki.

“Waliomleta waliamua kuhifadhi mwili wake katika hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo,” imeeleza taarifa hiyo.
 

Juni 12, 2019, Rais wa Tanzania, John Magufuli alimteua Dk Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Bharti Airtel International.

Katika makubaliano hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania pamoja na ofisa mkuu wa ufundi wanapaswa kuteuliwa na Serikali.

Kabla ya Dk Nundu  kuteuliwa alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com