Mwili wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyefariki dunia Ijumaa unasafirishwa leo kurejeshwa nyumbani kutoka Singapore kwa ajili ya mazishi.
Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 , alikuwa hospitalini kwa matibabu nchini Singapore.
Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zitafanyika siku ya Jumamosi , kabla ya kuzikwa kijijini kwao Jumapili.
Robert Mugabe, ambaye alikuwa kiongozi wa vita vya msituni ambaye aliiongoza Zimbabwe baada ya Uhuru mwaka 1980, aling'olewa madarakani mwaka 2017.
Social Plugin