Kwenzi kwa kawaida huwa tishio kwa waendesha baiskeli nchini Australia
Mwanamume mmoja raia wa Australia amefariki katika ajali ya baiskeli wakati akijaribu kukwepa ndege aina ya Kwenzi aliyekuwa akipepea juu yake.
Mwendesha baiskeli huyo mwenye umri wa miaka 76 alipata jareha la kichwa Jumpaili wakati alipopoteza muelekeo kutoka barabarani na kujigonga na uzio kusini mwa Sydney, polisi wamesema.
Licha ya jitihada za wahudumu wa afya kumuokoa, jamaa huyo alifariki alipofikishwa hospitalini baadaye.
Ndege hao kwa kawaida ni tishio nchini Australia wakati wa msimu wa machipuko na mara nyingi husababisha majeruhi kwa wanedesha baiskeli na hata wapita njia, lakinini nadra kwa waathiriwa kufariki.
Polisi wamesema watawasilisha ripoti ya mpasuaji maiti baada ya tukio hilo huko Wollongong, New South Wales.
Vyombo vya habari vimeripoti kwamba kumeshuhudiwa mashambulio mengine kadhaa ya ndege hao Kwenzi katika bustani kulikotokea ajali hiyo.
Kwenzi wa Australia ni tofauti na ndege wa Ulaya ambao wana jina sawa. Wakati wa msimu wa kujamiiana, ndege hao huwa wakali na huwashambulia binaadamu wanaopita katika maeneo wanakoishi.Ndege hao huwashambulia sana wakaazi wakati wa msimu wa machipuko
Mapema mwezi huu, serikali ya mtaa huko Sydney ilizusha mzozo wakati maafisa wa wanyama pori walipompiga risasi Kwenzi mkubwa, aliyewatishia wakaazi kwa miaka kadhaa.
Ndege huyo mkali aliwashambulia watu kadhaa na kusababisha baadhi kujeruhiwa na kupelelekwa hospitalini.
Mkazi mmoja pia alipatwa na mshtuko wa moyo baada ya kukabiliana na ndege huyo, shirika la habari nchini Australia linaripoti.
Maafisa kwa wakati huo, walitetea uamuzi wa kumuua Kwenzi huyo mkubwa. Ndege huyo hulindwa kwa sheria nchini lakini anaweza kudhibitiwa kwa hiari ya maafisa wa utawala.
Chanzo- BBC
Social Plugin