Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : AGAPE YAWAPIGA MSASA WALIMU WALEZI WA VILABU SHULENI KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI


Shirika lisilo la kiserikali la Agape Aids Control Programme la Mkoani Shinyanga, limeendesha mafunzo ya ukatili, na elimu ya afya ya uzazi na ujinsia, kwa walimu walezi wa vilabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni.

Mafunzo hayo yameendeshwa na shirika hilo la Agape, ikiwa ni sehemu ya kutoa mchango kwa Serikali katika mpango wa Taifa wa kutomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA), ambao umelenga kupunguza ukatili kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2022 kutoka asilimia 37.

Mafunzo hayo yametolewa leo Septemba 25, 2019 kwenye hoteli ya Liga iliyopo Shinyanga Mjini, katika kutekeleza mradi wa ‘UTU WA MSICHANA’ ambao unafadhiliwa na Shirika la Mundo Cooperante la nchini Hispania, utakaotekelezwa ndani ya mwaka mmoja kwenye kata hiyo ya Mwamala, ambao utakoma Aprili 2020.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo,Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola amewataka walimu hao kuwa wajasiri katika kumlinda mtoto wa kike ili wapate kutimiza ndoto zao, na kuachana na tabia ya uoga kwa kuogopa lawama ndani ya jamii, na kusababisha tatizo la mimba na ndoa za utotoni kuendelea kuwepo.

“Nawaomba walimu tushirikiane kutokomeza tatizo hili la mimba na ndoa za utotoni, muwe mnachukua hatua pale wanafunzi wanapopewa ujauzito ama kukatishwa masomo kwenda kuozesha ndoa ya utotoni, mtoe ushirikiano hadi Mahakamani, na siyo kuwaachia Polisi tu na hatimaye kesi kuishia njiani,” amesema Myola.

“Pia nyie kama walimu walezi wa vilabu mashuleni, toeni sana elimu kwa wanafunzi juu ya madhara ya kujihusisha kwenye mapenzi wakiwa katika umri mdogo, bali wahimizeni wajikite kwenye masomo yao ili wapate kutimiza ndoto zao, ambapo mambo hayo watayakuta ukubwani wakiwa tayari wanakazi zao,” ameongeza.

Aidha amewataka pia wazazi mkoani Shinyanga, kupenda kusomesha sana watoto wao wa kike ikiwa wana akili sana, na kubainisha kwa utafiti ambao wameufanya Shirika hilo la Agape, watoto wengi ambao wamekuwa wakipewa ujauzito ama kuozeshwa ndoa za utotoni, ni wale ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye masomo yao.

Kwa upande wake Afisa mradi huo wa ‘UTU WA MSICHANA’ Sophia Rwazo kutoka Shirika la Agape, amesema wameamua kuutekeleza kwenye Kata hiyo ya Mwamala, mara baada ya kufanya utafiti wa awali na kugundua kuwepo na tatizo la wanafunzi kupewa ujauzito pamoja na kulazimishwa kuozeshwa ndoa za utotoni.

Amesema mradi huo utakuwa ukitoa elimu ya madhara ya ukatili kwa wanawake na watoto, wakiwamo wazazi, walimu, wanafunzi, wazee wa kimila, dini, Mabaraza ya watoto ya Kata, Kamati za MTAKUWWA, pamoja na viongozi wote wa Serikali kwenye Kata hiyo, lengo likiwa ni kuwapatia uelewa na kupinga kabisa vitendo hivyo, ili jamii ipate kuishi salama pamoja na wanafunzi kutimiza ndoto zao.

Aidha amesema mradi huo pia utawawezesha elimu ya msingi na Sekondari kwa mfumo usio rasmi, kwa kuwapeleka vyuo vya ufundi stadi wasichana ambao ni wahanga wa mimba na ndoa za utotoni, pamoja na wale ambao wanaishi katika mazingira hatarishi ili kuweza kutimiza ndoto zao, ambazo zilitaka kuzimwa sababu ya kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Nao baadhi ya walimu hao akiwamo Yohani Tsere kutoka Shule ya Sekondari Kaselya Kata ya Mwamala, wameshukuru utolewaji wa elimu hiyo, na kutoa wito kwa Serikali, ifanyiwe Marekebisho Sheria ya ndoa ya mwaka 1971, ambayo imekuwa kikwazo kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni kwa kuruhusu mtoto kuolewa kwa ridhaa ya wazazi au Mahakama.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Mkurugenzi wa Shirika la Agape mkoani Shinyanga John Myola akizungumza na walimu walezi wa vilabu Mashuleni Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na kuwataka kutoa elimu zaidi kwa wanafunzi kujitambua na kuacha ngono katika umri mdogo ili wapate kutimiza ndoto zao. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Mkurugenzi wa Shirika la Agape Mkoani Shinyanga John Myola, akiwataka walimu wa Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kuwa wajasiri katika kumlinda mtoto wa kike katika kutimiza ndoto zao na kuacha kuogopa lawama ndani ya jamii kwa kutowashughulikia watu ambao wamekuwa wakiwapatia mimba wanafunzi na kuwaozesha ndoa za utotoni.

Afisa mradi wa UTU WA MSICHANA Kutoka Shirika la Agape Sophia Rwazo, akitoa mafunzo kwa walimu walezi wa Klabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga namna ya kupinga ukatili na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.

Afisa mradi wa UTU WA MSICHANA Kutoka Shirika la Agape Sophia Rwazo, akiendelea kutoa mafunzo kwa walimu walezi wa Klabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga namna ya kupinga ukatili na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.

Mwanasheria kutoka Shirika la Agape Suzy Mussa akitoa elimu ya ukatili.

Walimu ambao ni walezi wa vilabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya Shirika la Agape namna ya kupinga ukatili, pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye Kata ya Mwamala.

Walimu ambao ni walezi wa vilabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya Shirika la Agape namna ya kupinga ukatili, pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye Kata ya Mwamala.

Walimu ambao ni walezi wa vilabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya Shirika la Agape namna ya kupinga ukatili, pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye Kata ya Mwamala.

Walimu ambao ni walezi wa vilabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya Shirika la Agape namna ya kupinga ukatili, pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye Kata ya Mwamala.

Walimu ambao ni walezi wa vilabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya Shirika la Agape namna ya kupinga ukatili, pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata ya Mwamala.

Walimu ambao ni walezi wa vilabu mashuleni kutoka Kata ya Mwamala halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakiwa kwenye mafunzo ya Shirika la Agape namna ya kupinga ukatili, pamoja na kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwenye kata ya Mwamala.

Mwalimu Theodora Mdagachule kutoka Shule ya Sekondari Kaselya Kata ya Mwamala akichangia mada kwenye mafunzo.

Mwalimu Idrisa Sajoho kutoka Shule ya msingi Bunonga Kata ya Mwamala akichangia mada kwenye mafunzo.

Walimu wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Walimu wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Walimu wakiwa kwenye kazi ya vikundi.

Mwalimu Kaitira Leonard kutoka shule ya msingi Igegu Kata ya Mwamala, akiwasilisha kazi ya kikundi.

Mwalimu Yohani Tsere kutoka shule ya Sekondari Kaselya Kata ya Mwamala, akiwasilisha kazi ya kikundi.

Mwalimu Regina Thedeo kutoka shule ya msingi Ibanza Kata ya Mwamala, akiwasilisha kazi ya kikundi.

Picha zote Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com