Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amekemea tabia ya baadhi ya Makamanda wa Polisi nchini kujihusisha na shughuli za kisiasa kwa kile alichoeleza kuwa ni kinyume na Katiba ya nchi.
Akizungumza kwenye kikao chake na Wakuu wa Jeshi la Polisi wa Mikoa, IGP Simon Sirro amesema hata jeshi hilo linashangazwa na baadhi ya maafisa wake kujihusisha na siasa.
Sirro amesema, "baadhi yetu kujiingiza kwenye harakati za kisiasa si sahihi kwa mujibu wa katiba yetu, lakini kwa 'ushahidi' unashindwa kabisa kujua maadili yako unatakiwa kufanya nini kwenye umma."
"Ukifanya kitu ambacho jamii haitegemei, kila mtu anakushangaa na wala sio sifa, hata sisi wenyewe tunakushangaa, ukienda kuzungumza watu wanataka kuona unasema vitu vya msingi", ameongeza IGP Sirro.
Mapema mwezi uliopita Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha Jonathan Shanna alionekana akitumia baadhi ya salamu za chama cha siasa.
Social Plugin