Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Ndugu Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mama Mabeyo ambaye amefiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwake Msasani mara baada ya kufiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.PICHA NA IKULU
Social Plugin