Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MAGUFULI AZINDUA RADA MBILI ZA USAFIRI WA ANGA


Na Dianarose  Shirima-Maelezo.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amezindua RADA za usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICA) na uwanja wa ndege Kilimanjaro(KIA) ikiwa ni mwendelezo wa mradi uliokuwa umeanzishwa na serikali ya awamu ya tano kufuatia kuhamasisha safari za ndege na kuendeleza shirika la ndege la Tanzania(ATCL) uzinduzi huo umefanyika jijini Dar Es Salaam katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA). 


 Akizungumza na wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewapongeza wakandarasi toka Ufaransa waliopewa mradi huo na kuukamilisha mapema kama alivyohimisa hapo awali. 


Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic  Clavier, amesema Ufaransa inaunga mkono katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania kupitia viwanda na kusema kuwa Ufaransa ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuleta maendeleo na kufikia uchumi wa kati kwa maslahi mapana ya taifa la Tanzania. Balozi pia akampongeza Rais Dkt. Magufuli pamoja na watanzania kwa jinsi walivyoungana kwa pamoja ili kuleta maendeleo nchini kwa kasi. 


Katika uzinduzi huo, Dkt. Magufuli amewakaribisha nchi za Afrika na Ulaya kupitisha ndege zao katika anga la Tanzania kwa kuwathibitishia usalama katika anga la Tanzania na kuwataka wasiogope wao wapite katika anga la Tanzania na wataongozwa vizuri, Rais Magufuli amesema kuwa licha ya kuanzisha safari Mumbai, India serikali imelenga kuanzisha na nchi zingine pia duniani, ikiwemo China na London na kusisitiza kuwa zingine zitafuata. 


Aidha, Rais Magufuli amewataka watanzania kutokukata tamaa pale zinapotokea changamoto katika harakati za kuleta maendeleo,  akasema kuwa hata ndege  iliyokamatwa huko Afrika Kusini ni moja ya changamoto katika maendeleo, hivyo watanzania wanatakiwa kuwa na umoja hata pale changamoto zinapotokea bila kuangalia tofauti zao za kisiasa kwani maendeleo ya Tanzania hayana chama bali yatafaidisha kila mmoja hata wajukuu wa kizazi kilichopo sasa. 


Rais Magufuli amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza Johari, kutokana na uchapakazi mahiri aliouonesha katika nafasi hiyo, pia akasema kwa mwaka wa fedha uliopita, Mamlaka hiyo ilikusanya mapato ya Billioni 71 kutoka Billion 40  na kwamba mwaka ujao wa fedha wanatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Billioni 82. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com