Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kufungua mkutano mkuu wa 21 wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu mjini Arusha kaskazini mwa nchi hiyo.
Mkutano huo utashirikkisha wajumbe ambao ni ma Inspekta Jenerali wa Polisi kutoka nchi 14 za Burundi, Comorro, Djibouti, Congo Brazzaville, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia na Rwanda. Nyingine ni Ushelisheli, Sudan Kusini, Uganda, Eritrea, Sudan na mwenyeji Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, David Misime amesema kuwa, maandalizi ya mkutano huuo yamekamilika na kwamba, walianza kupokea wageni hapo jana.
Misime amesema pia kuwa, kabla ya kufanyika ufunguzi wa mkutano huo, kutakuwa na vikao vya wakuu wa vitengo vya Interpol vitakavyofanyika kuanzia kesho Jumapili tarehe 15 hadi tarehe 17 mwezi huu, kisha kufuatiwa na mkutano wa wakurugenzi wa upelelezi wa makossa ya jinai na kikao cha wajumbe wa kamati ndogo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania amesema pia kutakuwa na kikao cha kamati ndogo ya wataalamu wa sheria, vikao vya wajumbe wa kamati ya dawati la masuala ya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kikao cha wajumbe wa masuala ya kukkabiliana na ugaidi nchini.
Kwa mujibu wa Misime kaulimbiu ya mkutano huo ni "Kuimarisha Ushirikiano na Ubunifu Katika Kupambana na Uhalifu Unaovuka Mipaka" ambapo lengo hasa ni kuongeza ushirikkiano katika kukabiliana na makosa yanayovuka mpaka na kuwekka mikakati ya pamoja katika maazimio ya kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo.
Social Plugin