Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YASEMA HAKUNA UBAGUZI KATIKA UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI ELIMU YA JUU

Na.Faustine Gimu Galafoni ,Dodoma

BUNGE limeelezwa kuwa hakuna ubaguzi wowote katika utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwani hutolewa kwa wanafunzi watanzania wote wenye uhitaji na walioomba mikopo wa kuzingatia sheria taratibu na vigezo vilivyowekwa.

Hayo yamesemwa jana bungeni  na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  William Ole Nasha wakati alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Viti maalum (CCM) Halima Bulembo ambapo alisema kuwa ni vema waombaji wakazingatia maelekezo yanayotolewa na bodi wakati wa uombaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na kujaza taarifa zao kwa usahihi na kuambatanisha nyaraka zote muhimu.

Katika swali lake Mbunge Halima amesema kuwa  Je,ni kwanini mikopo ya wanafunzi wa chuo kikuu imekuwa ikitolewa kwa ubaguzi.

Akijibu swali hilo Mhe.Ole Nasha amesema kuwa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hotolewa kwa mujibu wa sheria ya bodi ya mikopo (sura 178) ambayo inabainisha  sifa za msingi.

Sifa hizo ni pamoja na awe mtanzania aliye dahiliwa katika masomo ya shahada katika taasisi inayotambuliwa na serikali,na asiwe na vyanzo vingine vinavyogaramia masomo yake,na kwa mwanafunzi anayeendelea na masomo awe amefaulu kuendelea na masomo katika mwaka unaofuata.

“Kwa mujibu wa sheria ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,bodi inamamlaka  ya kuweka utaratibu wa kubaini wahitaji,hivyo bodi huandaa mwongozo unaoweka masharti kwa waombaji pamoja na maelekezo juu ya mambo muhimu ya kuzingatiwa kwa waombaji ambao yatima,wenye ulemavu au wenye wazazi wenye ulemavu,na wale ambao masomo yao ya sekondari au stashahada yalifadhiliwa na maelekezo hayo ni pamoja na kuambatanisha uthibitisho wa hali zao”amesisitiza


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com