Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
WIZARA ya Kilimo imesema inapitia mfumo mzima wa usambazaji pembejeo za mazao ili kuondokana na ucheleweshaji na wizi unaoendelea ambao mwisho wa siku unasababisha mkulima kubeba mzigo huo.
Naibu Waziri wa wa wizara hiyo HUSSEIN BASHE amesema hayo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bunda BONIFAFE GETERE aliyetaka kujua kama wakulima wa pamba katika msimu 2019/2020 watakatwa fedha ya pembejeo.
Akijibu swali hilo BASHE amesema katika msimu huu wa kilimo mambo mengi yatabadilika katika usambazaji wa pembejeo.
Katika swali la msingi Mbunge wa Ukerewe JOSEPH MKUNDI amehoji mkakati wa serikali wa kufanya utafiti wa kisayansi ili kushauri wananchi wa Ukerewe aina ya mazao yanayopaswa kulimwa na jinsi ya kutumia eneo dogo la ardhi kwa ufanisi.
Akijibu swali hilo BASHE amesema Mkakati wa serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania{TARI} ni kufanya utafiti wa tabaka na afya ya udongo katika kanda zote saba za kiikolojia za kilimo nchini ikiwemo kanda ya Mwanza.
Social Plugin