Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Serikali inatarajia kutoa jumla ya Shilingi bilioni 33.5 kwa ajili ya kujenga wodi 2 katika kila hospitali 67 za wilaya zinaoendelea kujengwa nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa SELEMANI JAFO amesema hayo wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa katika kijiji cha Mlowa Barabarani.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo waziri JAFO amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na kuwahimiza kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameishukuru serikali kwa kuimarisha huduma za afya katika mkoa wa Dodoma.
Kwa upande wake mkurugenzi wa CHamwino ATHUMANI MASASI amesema Ujenzi huo ulianza februari mwaka huu kwa kupokea kiasi cha shilingi bilioni 1.5 na unatarajiwa kukamilika septemba 30 mwaka huu.
Ujenzi wa hospitali hizo ulihusisha jengo la maabara,jengo la wagonjwa kutoka nje,jengo la kuhifadhi dawa,jengo la mama na mtoto,utawala,jengo la mionzi na la kufulia nguo.
Social Plugin