Real Madrid na Barcelona zinatarajiwa kushindana pakubwa kuwania kumvutia meneja Jurgen Klopp na mlinzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Liverpool. (AS, kupitia Star)
Manchester United imejitolea kumfanya kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, kuwa mcheza soka anayelipwa pakubwa katika ligi kuu ya England katika kumshawishi kusaini mkataba mpya wa muda mrefu (Times)
Christian Eriksen anapuuzia mkataba mpya anaopendekezewa na Tottenham wakati wakala wa mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 27akishughulikia uhamisho kwenda Real Madrid msimu ujao wa joto. (Marca, kupitia Express)
Mchezaji wa kiungo cha mbele Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, na kipa Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 27, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid, baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Chelsea mwenye miaka 28, kuhusishwa na uhamisho kwenda Uhispania. (Sun)Eden Hazard, na kipa Thibaut Courtois, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid
Huenda Real Madrid ikamkabidhi mchezaji wa kiungo cha kati Toni Kroos, kwa Manchester United ili kwa upande wake ijipatie mchezaji wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 26 Paul Pogba. (FourFourTwo)
Arsenal inakaribia kufanikiwa kumsajili kijana wa Sunderland Logan Pye baada ya mchezaji huyo wa miaka 15 kuhusishwa ma uhamisho kwenda katika ligi kuu ya England wakati wa msimu wa joto. (Sun)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United, Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, yuko kwenye rada ya Juventus huku kukiwadia kinachowezekana kuwa ni mageuzi ya Januari. (Mirror)
Baada ya kuwasajili wachezaji 12 katika uhamisho wa msimu wa joto, mipango imeidhinishwa kwa Aston Villa kushughulika kwa mara nyingine katika dirisha la Januari. (Birmingham Mail)
Manchester United ilituma mawakala kumchunguza mshambuliaji wa Kosovo, Vedat Muriqi, mwenye umri wa miaka 25, wakati alipofunga dhidi ya timu ya England huko Wembley Jumanne usiku. (Express)
Meneja wa Arsenal, Unai Emery amefichua kwamba alikuwa na Javi Gracia wakati Watford ilipomfuta kazi. (Metro)
Bingwa wa Manchester United Gary Neville amesema anaweza 'kukimbia maili moja' iwapo atapewa kazi ya U meneja Old Trafford. (Manchester Evening News)
Tetesi za Jumapili
Mchezaji nyota wa zamani wa England, David Beckham ameongezea nguvu mipango yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Beckham anamiliki klabu ya soka nchini Marekani ijulikanayo kama Inter Miami, ambayo imeshatuma wawakilishi wake kuzungumza na baba wa Messi. (Sun on Sunday)
Inter Miami pia wanataka kumsajili winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale, 30.(Maxifoot - in French)
Manchester United wanapanga kumsajili kiungo Mjerumani wa klabu ya Real Madrid Toni Kroos, 29, mwezi Januari katika mkataba wa kubadilishana wachezaji.
United wanaweza wakamtoa Paul Pogba na kukubali kiasi cha pesa kama sehemu ya makubaliano hayo. (Bild - in German)
Kipa wa Uhispania David de Gea, 28, ametia saini mkataba mpya wa miaka minne na Man United wa thamani ya pauni 250,000 kwa wiki, na malipo yanaweza kupanda mpaka pauni 350,000 kwa wiki kulingana na kiwango cha mchezo. (Sunday Mirror)
Mshambuliaji wa England Callum Hudson-Odoi, 18, anatarajiwa kuingia makubaliano mapya na klabu yake ya Chelsea mara baada ya kupona majeraha yake. (Sun on Sunday)
Liverpool wameanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na mshambuliaji wake raia wa Senegali Sadio Mane. (SoccerLink, via Sport Witness)
Kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, anasubiria uwezekano wa kuihama klabu ya Tottenham na kuelekea Real Madrid, mwezi Januari. (Marca - in Spanish)
AC Milan na Inter Milan wote wana mipango ya kumsajili kiungo Mserbia Nemanja Matic, 31, kutoka Manchester United mwezi Januari. (Corriere Dello Sport - in Italian)
Manchester United wametuma wachunguzi wake kumuangalia mshambuliaji wa Fenerbahce ya Uturuki Vedat Muriqi, 25, wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Kosovo dhidi ya England wiki iliyopita. (Sunday Express)
Kocha wa Newcastle Steve Bruce amepewa ridhaa na uongozi wa klabu ya kusajili wachezaji wapya mwezi January, hususani mawinga. (Chronicle)
Mshambuliaji wa Juventus na Croatia Mario Mandzukic, 33, ambaye alikuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Man United hivi karibuni, anakaribia kukamilisha usajili wa kuelekea Marekani katika klabu ya LAFC. (Calciomercato)
Beki raia wa England Tyrone Mings, 26,amesema alishangazwa sana pale Aston Villa walipoamua kumsajili kwa pauni milioni 20 kutoka klabu ya Bournemouth. (Express and Star)
Chanzo -BBC
Social Plugin