Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SOKWE AZAA MTOTO BAADA YA DAWA ZA 'KUPANGA UZAZI' KUSHINDWA KUFANYA KAZI

Sokwe anayeishi katika hifadhi moja ya wanyama nchini Uganda amezaa mtoto ambaye "hakumtarajia" baada ya dawa za kupanga uzazi alizokua akitumia kushindwa kufanya kazi, maafisa wameiambia BBC.

Wasimamizi wa hifadhi ya wanyama ya Ngamba Island katika eneo la ziwa Victoria walipigwa na butwaa baada ya kugundua sokwe huyo ana mimba na kuongeza kuwa wanafanya uchunguzi wa chembe chembe za vinasaba kubaini baba wa mtoto wake.

Sokwe huyo anaefahamika kama Natasha, ambaye anakadiriwa kuwa na miaka 29 aliokolewa kutoka eneo la Arua magharibi mwa Uganda karibu miaka 21 iliopita.
Msimamizi wa hifadhi hiyo anasema walijaribu kumsaidia sokwe huyo asizae mtoto kwasababu hawana uwezo wa kumlea.

''Sawa na binadamu, sokwe wa kike wanatumia dawa za kupanga uzazi ili kujilinda na mimba zisizotarajiwa. Mbinu hii hutumiwa kudhibiti idadi ya sokwe katika hifadhi hiyo iliyotengwa kuwatunza wanyama mayatima,'' Titus Mukungu, ambaye pia ni daktari wa wanyama, aliiambia BBC.

Sokwe Natasha alikua n a watoto wanne waliozaliwa miaka 20 iliopita, kumaanisha kuwa dawa za uzazi wa mpango zinafanya kazi, alisema.

Sokwe huyo mchanga aliyezaliwa Septemba 5 imefikisha 50 idadi ya sokwe katika hifadhi hiyo Ngamba Island.

Shirika moja la mazingira limetoa wito kwa watu kumpatia jina mwanasokwe huyo mchanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com