Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : TAMASHA LA 14 LA JINSIA LAFUNGULIWA JIJINI DAR ES SALAAM..ANGALIA MATUKIO YOTE YALIYOJIRI HAPA

Balozi Getrude Mongella ambaye ni Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) na Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa wanawake duniani uliofanyika mwaka 1995 Beijing China amefungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 leo Jumanne Septemba 24,2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kufungua Tamasha hilo litakalodumu kwa muda wa siku nne (Septemba 24 hadi 27,2019),Balozi Mongella maarufu 'Mama Beijing' amesema ili kujenga Tanzania ya Viwanda ni lazima wanawake na wanaume washiriki.

Balozi Mongella pia amehamasisha umuhimu wa wanawake kushirikishwa katika utengezaji wa Ilani za uchaguzi za vyama vya siasa ili kuhakikisha masuala ya wanawake yanaingizwa kufikia usawa wa kijinsia.

"Huu msemo wa Wanawake wakiwezeshwa wanaweza mimi nasema hii ni dhambi...hatupaswi kuwa omba omba...Sisi wanawake tunaweza tunachotaka ni vikwazo vinavyotukwamisha viondolewe njiani,tunataka wanawake washiriki kwenye utengenezaji wa ilani za uchaguzi ili Rais atakayegombea apewe na kubeba ajenda zinazohusu wanawake",alisema Balozi Mongella.

"Tuone masuala yanayotuhusu wanawake ni sehemu ya ajenda na uchaguzi utakapopita iwe rahisi kwa tutakayemchagua kuwa Rais kumuomba akimbizane na ajenda za wanawake na asipofanya hivyo atakuwa hajatekeleza Ilani",aliongeza Mama Mongella.

Hata hivyo aliipongeza serikali kwa kutekeleza ajenda za Mkutano wa Beijing mfano Sera ya elimu bure hali inayosababisha ongezeko la watoto wa kike kwenda shule na imeondoa kikwazo cha watoto kukosa elimu.

Aidha Balozi Mongella aliwataka wanasiasa kuepuka Rushwa huku akieleza kuwa Wanasiasa wanaohonga 'rushwa' ili wapate uongozi wanabaka siasa.

Naye Mgeni Maalumu kutoka serikalini,Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alisema Ukatili wa Kijinsia ni janga jipya linaloitia doa nchi ya Tanzania hivyo kuwaomba wadau wote kuungana kutokomeza hali hiyo.

"Hatuwezi kufikia usawa wa kijinsia katika taifa kama tunaendelea kuwa na matukio ya ukatili ya kijinsia ambayo nyuma yake yana sura ya mila,desturi,umaskini na ukosefu wa elimu.Naomba tuvunje ukimya na tuepuke kumaliza kesi zinazohusu masuala ya ukatili kwa kuyamaliza kienyeje",alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019.

Akielezea kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia 2019,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi alisema linahudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake kutoka ndani na nje ya Tanzania likiongozwa na mada kuu 'Wanaharakati wa jinsia mbioni kubadili dunia'.

"Tamasha hili lina umuhimu wa kipekee kwani tunaendelea kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya TGNP tangu ianzishwe mwaka 1993 na kidunia tumeanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio na Mpangokazi wa Beijing ambapo kilele chake ni mwaka 2020",alisema Liundi.

ANGALIA HAPA CHINI PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI
Balozi Getrude Mongella akifungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Balozi Getrude Mongella akifungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019.
Balozi Getrude Mongella akisalimiana na Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kufungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. 
Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Awali Balozi Getrude Mongella (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro wakifurahia jambo wakati akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Meza kuu wakiwa wamesimama baada ya Balozi Getrude Mongella kuwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam.
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 wakiendelea na burudani wakati Balozi Getrude Mongella akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua tamasha hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
MC wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 ambaye ni Mwanachama wa TGNP Mtandao Usu Mallya akitoa maelekezo mbalimbali wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wa tamasha.
Sehemu ya wageni waalikwa wakati wa tamasha hilo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania,Anne Makinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Waziri Mkuu Mstaafu Tanzania,Joseph Sinde Warioba akizungumza wakati wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Washiriki wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 wakicheza muziki.
Washiriki wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo.

Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 likiendelea.

Mwakilishi wa balozi wa Ireland nchini akizunguza kwenye tamasha la 14 la jinsia 2019
Mwakilishi Mkazi Un Women nchini Tanzania akizunguza kwenye tamasha la 14 la jinsia 2019

Utoaji Tuzo maalum kwa viongozi wa serikali ambao wamechangia mabadiliko ya kisera kuwezesha masuala ya kijinsia kufanikiwa ikiwemo utekelezaji wa maazimio ya Beijing mwaka 1995.Kushoto ni Afisa Programu Mwandamizi TGNP Mtandao,Deogratius Temba akishikana mkono na Balozi Getrude Mongella baada ya kupokea cheti kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Benjamin Mkapa ambaye wakati wa uongozi wake aliweka mazingira wezeshi kupokea na kusaidia utekelezaji wa maazimio ya Beijing 1996.
Balozi Getrude Mongella akikabidhi tuzo kwa Mhe. Joseph Sinde Warioba ambaye ametunukiwa tuzo ya heshima kwa sababu kwa muda mrefu amekuwa mstari wa mbele kusimamia ajenda ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia kila mahali anapokuwa.
Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro akimkabidhi Balozi Getrude Mongella tuzo ya heshima kwa kumtambua kuwa mwanamke shupavu anayesimamia haki za wanawake na usawa wa kijinsia bila kutetereka.
Bhoke Wankyo Nyerere akipokea Tuzo ya Heshima iliyotolewa kwa hayati Baba wa taifa kama sehemu ya kuendeleza kuuenzi mchango wake katika kutetea,kulinda na kupigania haki za watu wote zikiwemo za wanawake na usawa wa kijinsia.
Tuzo ya heshima kwa Hayati marehemu Sophia Kawawa ikitolewa ikiwa ni tuzo ya heshima kuuenzi mchango wake katika kupigania haki za wanawake hasa waajiriwa.
Agripina Mosha akipokea kwa niaba ya Dr. Inj. Strato Mosha tuzo ya heshima kwake kwa kujitoa tangu awali kabisa wakati shirika la TGNP linaanza.
Mwakilishi wa Prof. Simon Mbilinyi akipokea tuzo ya heshima kwa kujitoa kwake kwa rasilimali na wakati mwingine ushauri
Utoaji tuzo kwa watu binafsi ambao walitumia rasilimali zao,muda,ushauri,kuwezesha TGNP Mtandao kusimama na kufika hapo ilipo sasa.
Mwakilishi,akipokea tuzo ya heshima kwa Marehemu Prof. Seth Chachage
Dkt. Hellen Kijo Bisimb akionesha tuzo ya heshima aliyopewa kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya shirika la LHRC.
Vicky Tetema kutoka Under the Same Sun akipokea tuzo kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya shirika hilo.
Mary Lusindi akipokea tuzo kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya TGNP.
Usu Mallya akioesha tuzo ya heshima aliyopewa kutokana na kuendeleza agenda ya ukombozi wanawake kimapinduzi ndani ya TGNP
Usu Mallya akipiga picha na Mkurugenzi wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi baada ya kupewa tuzo ya heshima.
Perpetua Magoka akipokea tuzo ya heshima kwa niaba ya WLC
Utoaji tuzo ukiendelea
Mwakilishi wa halmashauri ya Kishapu akipokea tuzo kutokana na halmashauri hiyo kutenga fedha kwenye bajeti zake mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mrengo wa kijinsia baada ya kujengewa uwezo na TGNP Mtandao.Halmashauri hiyo pia imetenga bajeti kuwezesha wasishana waliopo shuleni kupata taulo za kike bure wanapozihitaji.
Mwakilishi wa halmashauri ya Kisarawe akipokea tuzo kutokana na halmashauri hiyo kutenga fedha kwenye bajeti zake mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mrengo wa kijinsia baada ya kujengewa uwezo na TGNP Mtandao.Halmashauri hiyo pia imetenga bajeti kuwezesha wasishana waliopo shuleni kupata taulo za kike bure wanapozihitaji.
Mwakilishi wa halmashauri ya Morogoro akipokea tuzo kutokana na halmashauri hiyo kutenga fedha kwenye bajeti zake mwaka wa fedha 2019/2020 kwa mrengo wa kijinsia baada ya kujengewa uwezo na TGNP Mtandao.Halmashauri hiyo pia imetenga bajeti kuwezesha wasishana waliopo shuleni kupata taulo za kike bure wanapozihitaji.
Mwakilishi wa UN Women nchini Tanzania akipokea tuzo ya heshima
Mwakilishi wa Sweden nchini Tanzania,Anders Sjoberg akipokea tuzo ya heshima
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao akipokea tuzo ya heshima kwa kupigania masuala yanayohusu wanawake.
Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakipiga picha ya pamoja baada ya mkurugenzi wa TGNP Mtandao kupokea tuzo.
Wafanyakazi wa TGNP Mtandao wakipiga picha ya pamoja baada ya mkurugenzi wa TGNP Mtandao kupokea tuzo.
Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kufungua maonesho kwenye Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. 
Picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com