Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ametimiza ahadi yake kwa Mama wa Mapacha kwa kumjengea nyumba yakuishi baada ya ile ya awali iliyokuwa haina mazingira mazuri ya kuishi, Jokate amesema watamkabidhi mama huyo nyumba hiyo ambayo inavyumba viwii vyenye tiles, umeme, choo, jiko na mahitaji mengine ya msingi.
Kupitia ukurasa wake wa facebook DC Jokate ameshare habari hiyo kwa kuambatanisha muonekano wa picha za nyumba ya awali na ya sasa aliyomjengea kwa kushirikiana na baadhi ya makampuni waliojitolea.
”Naomba Mungu aendelee kututumia sisi viongozi na watumishi wake kuweza kugusa na kubadilisha maisha ya watu wengi zaidi. Tujitoe zaidi kuliko kufikiria maslahi yetu binafsi. Hatimaye ahadi tuliyotoa kwa mama wa mapacha waliotenganishwa Muhimbili imetimia. Na leo tunaenda kumkabidhi nyumba mpya ya kisasa ya vyumba viwili yenye tiles, umeme, choo, jiko na mahitaji mengine ya msingi. Ukilinganisha na nyumba ya awali aliyokuwa akiishi ya makuti kule Kimalamisale.
"Kipekee nawashukuru ubatanzania kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya kusimamia ujenzi kwa kutoa fedha za ujenzi na africanreflectionsfoundation kwa kushirikiana na Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya katika kununua kiwanja. Kwahiyo nyumba na kiwanja ina hati yenye majina ya watoto mapacha. Nimshukuru pia Michael Afisa Tarafa Mzenga kwa kusimamia vizuri ujenzi na mafundi wote walioshiriki. .Tukutane Mzenga leo kwenye makabidhiano.” Ameandika Jokate
Social Plugin