Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akionesha tuzo ya elimu aliyopewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwake ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka tuzo ya elimu iliyotolewa na Taasisi hiyo kwake ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Komredi Enock Yakobo akionesha tuzo ya elimu iliyotolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye tuzo ya elimu iliyotolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
****
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Mkoa wa Simiu, Mhe. Anthony Mtaka amepewa tuzo ya elimu ya Tanzania Elimu Awards na Taasisi ya Elimu Solutions, ikiwa ni kutambua mchango wake kama kiongozi aliyefanya vizuri na mwenye mchango mkubwa katika mapinduzi ya elimu Mkoani Simiyu.
Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Solutions, Neithan Swed, Mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliopata ufaulu hafifu(daraja sifuri) katika mtihani wa Mock kwa lengo la kuwasaidia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Novemba 2019.
Swed amesema Taasisi hiyo imefuatilia na kuona juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu katika mapinduzi ya elimu ikiwemo ubunifu wa kuanzisha kambi za kitaaluma ambazo zimeonekana kuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ufaulu wa mkoa wa Simiyu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutoka mwaka 2016 hadi mwaka 2018.
“Anayoyafanya Mhe. Mtaka hayaishii Simiyu peke yake Tanzania inayaona, tulifuatilia habari za kambi za kitaaluma na tukaangalia nafasi ya mkoa katika matokeo na namna mlivyofanya vizuri, mmeweka alama kwenye Taifa na tunatamani Mhe. Mtaka aziendeleze juhudi hizi zaidi ili mtoke kwenye kumi bora mwende tatu bora na mwakani tupate mwanafunzi bora kutoka Simiyu atakayepata tuzo hii” alisema Neithan Swed.
Katika hatua nyingine Swed amesema Taasisi ya Elimu Solutions itatoa ufadhili kwa mwanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2019 atakayefanya vizuri katika mtihani wa Taifa na kumpeleka nchini China kuendelea na masomo.
Akipokea tuzo hiyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Taasisi ya Elimu Solutions kwa kutambua juhudi zinazofanywa na mkoa wa Simiyu na kutoa tuzo huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaithamini sana tuzo hiyo.
Aidha, Mtaka ameipongeza Taasisi ya Elimu Solutions namna wanavyohamasisha maendeleo ya Elimu ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenda kusoma nje ya nchi.
Tuzo za Elimu Tanzania Elimu Awards zimetolewa na Taasisi ya Elimu Solutions kwa wadau mbalimbali wa elimu waliochangia na kusaidia kuleta mabadiliko kwa ubunifu na juhudi zao binafsi, taasisi zinazoihudumia sekta ya elimu; pia hutolewa kwa viongozi, walimu, wanafunzi waliofanya vizuri kwenye elimu.
Social Plugin