Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Leonard Chamriho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board).
Dkt. Chamriho ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Rais Magufuli amewateua wajumbe wanne wa bodi hiyo ambao ni;
Dkt. Chamriho ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Rais Magufuli amewateua wajumbe wanne wa bodi hiyo ambao ni;
- Casmir Sumba Kyuki (Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria).
- Dkt. Suleiman Magesa Missango (Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania – BOT).
- Safiel Fahamuel Msomvu (Kaimu Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania – TPDC).
- Dkt. Mussa Daniel Budeba (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Chamriho na Wajumbe hao umeanza tarehe 25 Septemba, 2019.
Social Plugin