Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amewataka wananchi wanaoishi ndani vijiji 11 halmashauri ya mji wa Njombe vilivyokosa umeme kuwa wavumilivu kwani serikali inategemea kufikisha umeme katika vijiji hivyo ndani ya miezi minne.
Waziri Kalemani wakati akiwasha umeme Kituo cha afya cha Ihalula kilichopo kata ya utalingolo halmashauri ya mji wa Njombe amesema,jimbo la Njombe mjini lina vijiji 44,vitongoji 29 huku vijiji 11 pekee vikikosa umeme.
“Hii ni Njombe mjini na sio Njombe vijijini kwa maana hiyo haikuwemo kwenye mpango wa umeme vijijini,lakini serikali imemsikiliza Mbunge wa hapa,umeme ulikuwa ni wa laki tatu na ishirini,ulikuwa ni wa laki moja na sabini na saba ila leo mnalipa elfu 27,na mbunge wa hapa ana vijiji 44 na vitongoji 29 katika vijiji 44 vijiji 11 vilivyobaki havijapelekewa umeme navyo vitapelekewa ndani ya miezi minne”alisema Kalemani
Mbunge wa jimbo la Njombe mjini Edward Frans Mwalongo amesema jimbo lake licha ya kutokuwepo kwenye mpango wa umeme wa rea lakini serikali imepeleka umeme huo huku akiomba vijiji vyote vilivyosalia vipatiwe umeme pamoja na kuwaangalia kwa ukaribu wazalishaji binafsi wa umeme wa maporomoko ya maji.
“Lakini mh.waziri nikuombe sana wako wafuaji wa umeme binafsi.niwaombe kama wizara na kama tanesco,muwasimame wafanye kazi kwa mwendo unaolidhisha kwasababu wengine wamechukuwa mda mrefu sana kuzifanya hizo kazi bila mafanikio makubwa na wananchi wanahitaji umeme”alisema Mwalongo
Baadhi ya wakazi wa Ihalula wamesema kufika kwa umeme huo kutawasaidia kufungua miradi mbalimbali ya kiujasiriamali kama viwanda vidogo vidogo vya kusindika nafaka na matunda.
Hata hivyo waziri Kalemani amefika na kuwasha umeme kijiji cha Itombololo kata ya Igima,Itowo kata ya Mdandu na kijiji cha Saja vilivyopo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.
Social Plugin