Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba, Mhe. Hashimu Murshid Ngeze akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani
Na Lydia Lugakila - Malunde 1 blog
Halmshauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera imetoa shilingi milioni 121 kwa ajili ya kuwezesha vikundi 26 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika kipindi cha mwaka 2018/2019.
Kauli hiyo imetolewa leo Sepemba 5,2019 na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bukoba mkoani Kagera,Mhe. Hashimu Murshid Ngeze katika kikao cha Baraza la madiwani cha kufunga mwaka 2018/2019 kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
Ngeze amesema kuwa mikopo hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 121 imetolewa kwa ajili ya kuwezesha vikundi 26 ikiwemo 26 ambapo kati ya vikundi hivyo 8 ni vya vijana, wanawake 15 na vitatu vya watu wenye ulemavu na kuitaja halmashauri hiyo kupiga hatua kubwa katika kuyakwamua makundi mbal mbali kwani miaka ya nyuma kiwango hicho hakijawahi kufikiwa.
Amesema ili kuendelea kuona umuhimu huo katika vikundi hivyo halmashauri hiyo imeendelea kutoa elimu ya ujasiriamali kwa lengo la kuwawezesha wananchi kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao kwa urahisi na kuwa mafunzo hayo yamefanywa kupitia vikundi vya kijamii kwa kata zote 29.
Amesema matarajio kwa mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri hiyo itaendelea kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na wananchi ili wananchi waweze kutambua mifuko mingine inayoweza kuwasaidia katika kupata mikopo na hatimaye waweze kujianzishia viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ya Tanzania ya viwanda.
Katika hatua nyingine Ngeze amesema Halmashauri hiyo imepiga hatua kubwa katika kunusuru kaya maskini kupitia mpango wa TASAF III awamu ya kwanza kwani jumla ya kaya vijiji 63 na kaya 8061 zimeendelea kunufaika na lengo la TASAF III awamu ya pili ni kuhakikisha kuwa vijiji na kata 903 pamoja na maafisa ugani 70 katika kata 14 na tayari wamepewa mafunzo juu ya sheria za ardhi na mpango wa urasimishaji ardhi kwa ktumia upimaji shirikishi na upangaji wa miji.
Kwa upande wao,madiwani wa halmashauri wamesema wataendelea kupigania masuala ya kimaendeleo ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi wao na kuhimiza uchangiaji wa miradi ya maendeleo.
Social Plugin