WAANDISHI WA HABARI TANZANIA WAOMBA SERIKALI KUREKEBISHA SHERIA KANDAMIZI

Rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo akizungumza wakati wa Mkutano mkuu wa UTPC.

Rais wa Muungano wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratias Nsokolo ameiomba Serikali ya Tanzania kutazama upya sheria ya huduma za habari ya 2016 na sheria ya mtandao kwani siyo rafiki kwa waandishi.

Nsokolo ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 7, 2019 katika hotuba yake kwenye mkutano Mkuu wa UTPC unaofanyika Visiwani Zanzibar.

Mkutano huo umehudhriwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri.

"Tunaomba Serikali ya Muungano kupitia Bunge ipitie upya sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 na sheria ya mtandao ambazo zimekuwa ni kikwazo kwa waandishi," amesema Nsokolo.

Nsokolo ameiomba serikali kuwasaidia waandishi ambao wamekuwa wakikutana na vipigo na manyanyaso katika maeneo yao ya kazi ili wafanye kazi zao kwa uhuru.



Na Habel Chidawali

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post