Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Mhe.Seleman Jafo ameziagiza Halmashauri Kote nchini kuwa na Mpango mkakati wa Kukutana na Taasisi za Dini angalau Mara mbili kwa Mwaka katika kujadili Mambo mbalimbali kwani Taasisi hizo zimekuwa na mchango mkubwa kwa Taifa .
Waziri Jafo ameyasema hayo jijini Dodoma Sept.4,2019 wakati akifunga mkutano wa 82 wa chama cha Madaktari wa kikristo Tanzania [TCMA] ambapo amesema miongoni mwa watu Muhimu katika Taifa lolote lile ni Madaktari na walimu ,hivyo viongozi wa Dini ni Walimu muhimu wanaosaidia kuelimisha jamii kuwa na maadili mema na Msingi Bora wa kuishi ikiwa ni Pamoja na kuepuka matendo maovu ya dawa za kulevya ,Wizi,Uvivu na Ugaidi.
Kutokatana na hilo Waziri Jafo ameagiza Halmashauri kote nchini Kufanya vikao na viongozi wa Dini angalau Mara mbili kwa Mwaka ili kuweza kujadili mambo muhimu ya Kujenga Taifa.
”Kati ya watu muhimu katika Taifa hili na Duniani kote ni Madaktari na Walimu,Ninyi viongozi wa Dini ni Walimu wazuri mnaobadilisha Tabia mbovu ya watu na kuwa na tabia nzuri .Kuna suala la utoaji wa huduma na Taasisi za kidini zimekuwa zinafanya vizuri,kwa hiyo tu mimi niagize halmashauri kote nchini kuwa na desturi ya kukutana na Taasisi za dini angalau mara mbili kwa mwaka katika kujadili changamoto mbalimbali kwani ninyi mmekuwa msaada kubwa kwa serikali”alisema.
Aidha,Waziri Jafo ameipongeza TCMA Kwa kuzindua kampeni ya “Zijue Namba zako kwa Afya yako “kwani itakuwa chachu kubwa kuelimisha jamii kuhusu masuala ya Afya hususan Elimu ya Magonjwa yasiyoambukiza ambayo yameshamiri kutokana na ulaji usiozingatia Kanuni za bora za Afya hali inayopelekea kuwa na vitambi na Matatizo ya shinikizo la damu[Presha].
“Kati ya maeneo yenye changamoto kubwa ni Magonjwa yasiyo ya kuambukiza watu wanakula Mapochopocho wanafikiri unene ni Fashion ,na gharama ya matibabu kwa magonjwa yasiyoambukiza imekuwa ni kubwa .Kwa hiyo niwapongeze kwa kuzindua kampeni hii ya “zijue namba zako kwa afya yako” lengo ni kutoa elimu juu ya kuzingatia Kanuni bora za afya,na sijaona mtu mwenye kitambi humu”alisema.
Rais wa chama cha Madaktari Tanzania Bwire Chilangi amewasilisha mapendekezo kwa serikali ikiwa ni pamoja halmashauri kuelekeza kujaza nafasi za watumishi katika hospitali za kidini ambazo zina upungufu,kila kituo cha afya kuwa na akaunti ili kuepuka uchelewashaji wa fedha,halmashauri kuzingatia Geografia na eneo husika katika hospitali za kidini na kupitia huduma zinazotolewa kwendana na uhalisia.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya kidini ya Christian Social Services Comission[CSSC]inayosimamia sekta Afya na Elimu kwa Baraza la Maaskofu Makatoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania,Peter Maduki amesema Makanisa yataendelea kutoa huduma ya Afya na elimu bila ubaguzi milele na milele pamoja na kufuata kanuni na taratibu za serikali na Matumizi mazuri ya Rasilimali Fedha.
Chama cha Madaktari wa kikristo Tanzania [TCMA] Kimetimiza takribani Miaka 82 tangu kianzishwe mwaka 1937 ambapo chama hicho kinamiliki hospitali mbalimbali za Rufaa ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Social Plugin