Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WEZI WAIBA CHOO CHA DHAHABU


Choo cha dhahabu chenye karati 18 kimeibwa katika wizi wa mabavu usiku wa kuamkia leo katika Jumba la Blenheim

Genge moja lilivunja na kuingia katika kasri la Oxfordshire na kuiba kiti hicho , kulingana na maafisa wa polisi wa Thames Valley.

Kiti hicho kwa jina America , ambacho wageni wameombwa kukitumia hakijapatikana lakini mzee mmoja mwenye umri wa miaka 66 amekamatwa.

Wizi huo ulisababisha uharibifu mkubwa kwa kuwa choo hicho kilikuwa kimejengwa kushikana na msingi wa nyumba hiyo, polisi walisema.

Kilikuwa miongoni mwa vitu vya maonyesho ya msanii mmoja wa Itali Maurizio Cattelan yaliofunguliwa siku ya Alhamisi.

Jumba hilo ni la karne ya kumi na nane na eneo alilozaliwa Sir Winston Churchill. Kwa sasa limefumngwa huku uchunguzi ukiendelea.

Akizungumza mwezi uliopita nduguye wa kambo wa Churchil , Edward Spencer alisema kwamba hakuwa na shaka kuhusu usalama wa choo hicho. ''Sio kitu cha rahisi kufikiria''kasri la Blenheim limefunga huku poliksi wakifanya uchunguzi

Wageni katika jumba hilo la maonyesho walikuwa huru kutumia vifaa vya kasri hilo kwa malengo yake huku wakipewa muda wa dakika tatu ili kuzuia milolongo mirefu

Inspekta wa polisi Jess Milne alisema: Sanaa ilioibiwa ni kiti chenye thamani ya juu kilichotengezwa na dhahabu ambacho kilikuwa katika maonyesho hayo.

Tunaamini kwamba waliotekeleza kitendo hicho walitumia magari mawili wakati wa kisa hicho.

Kiti hicho hakijapatikana lakini tunafanya uchunguzi kukitafuta ili kuwakamata waliohusika.

Maafisa wa polisi wa Blenheim wanasema kwamba jumba hilo litaendelea kufungwa lakini litafunguliwa siku ya Jumapili.

Rais Donald Trump aliombwa kuchukua kiti hicho mwaka 2017. Mshukiwa kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa maafisa wa Polisi.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com