Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amepokea wanachama wapya 98, wa vyama vya CCM na CUF kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam walioamua kuachana na vyama vyao kwa malengo ya kuunga mkono chama hicho.
Hayo yamejiri jana wakati kiongozi huyo akiwapokea wanachama hao wapya na kusema kuwa sifa ya chama bora ni kile ambacho kina idadi kubwa ya wanasiasa na ugeni huo unaashiria ukuaji na ukomavu wa chama hicho.
''Jumla ya wenyeviti 38 wa mitaa, pamoja na wajumbe wao wametoka CUF na leo hii pia tumekabidhii kadi kwa baadhi yao, lakini pia tumekabidhi kadi kwa wenyeviti wa mitaa waliotoka chama cha CCM 52 ,wao walikuwa kwenye kura za maoni na kuna watu hawakutendewa haki, wameona kimbilio la haki ni kukimbilia ACT - Wazalendo na sisi tumewakaribisha sana'' amesema Zitto.
Aidha Zitto ametoa wito kwa vyama vya upinzani, ambavyo viko tayari kushirikiana na kuachiana wagombea kwa baadhi ya maeneo, wakutane na kuzungumza na kuweka makubaliano ya pamoja ili waweze kutimiza adhma yao ya kukiondoa cha tawala madarakani.
Social Plugin