Afisa mtendaji wa Kata Syridion Michael (40) mkazi wa kinondoni amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni kwa kosa la kujeruhi.
Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya hakimu Happiness Kikoga na Wakili wa Serikali Ester chale alidai Agosti 1, 2019 eneo la kinondoni mkwajuni wilayani kinondoni Dar es salaam alimng’ata upande wa kulia wa mdomo mtu mmoja Tanya Tasaluko na kumsababishia maumivu.
Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hili na wakili wa serikali alidai upelelezi wa shauri hili hauja kamilika aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa na kwa kukamilisha upepelezi.
Hakimu Kikoga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho vya taifa na kusaini bondi ya sh 500,000.
Hata hivyo mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yake itakuja kwa kutajwa tena octoba 15 mwaka huu.
Social Plugin